Utafiti: Maambukizi ya Corona ni mengi kuliko yanayoelezwa
9 Aprili 2020Watafiti wanasema kufikia sasa ni asilimia 6% tu ya mambukizi hayo ambayo yamegundugulika. Kulingana na utafiti huo, Christian Bommer na Sebastian Vollmer wa chuo kikuu cha Göttingen Ujerumani, wamechunguza data za gazeti la kila mwezi la Lancet ambalo hutoa taarifa kuhusu magonjwa ya kuambukizwa.
Kulingana na watafiti hao, data hizo zilionyesha kuwa huenda mataifa yamegundua tu asilimia 6% ya maambukizi hayo. Wanasema idadi jumla ya virusi vya Corona yumkini imependukia mamilioni kote duniani. Wanasema kufikia sasa huenda virusi vya Corona vimeshawaambukizi mamilioni ya watu duniani. "Matokeo haya yanamaanisha kuwa serikali zote na watungaji sheria wanapaswa kuwa makini sana wakati wakitoa idadi ya visa vya maambukizi ili waweze kurahisishwa katika kupanga mikakati ya kushughulikia visa hivyo. "Alisema Vollmer, profesa wa idara ya Maendeleao na Uchumi katika chuo hicho.
Makumi ya mamilioni ya mambukizi
Utafiti huo unakadiria kuwa kufikia Machi 31, 2020, Ujerumani ilikuwa na visa vipatavyo 460,000 vya mambukizi ya virusi vya Corona. Aidha unabaini kuwa siku hiyo hiyo Marekani ilikuwa na zaidi ya milioni 10 ya maambukizi hayo, huku nchini Uhispania wakikadiria kuwa tayari kulikuwa na watu milioni 5 wenye virusi hivyo. Huko Italia, nchi ambayo sasa ni kiini cha virusi hivyo, watafiti wanasema ilikuwa na visa vipatavyo milioni 3 kufikia Machi 31 huku Uingereza ikiwa na maambukizi milioni 2.
Kwa mujibu wa data za chuo kikuu cha John Hopkins, iliripoti kutokea kwa visa 900,000 vya maambukizi kote duniani siku hiyo. Watafiti Christian Bommer na Sebastian Vollmer wameeleza kuwa wakati data za chuo kikuu cha Johns Hopkins zikieleza kutokea kwa maambukizi chini ya milioni moja mnamo Machi 31, wanakadiria kuwa tayari kuliwa na mamilioni ya maambukizi. Utafiti huo unaeleza.
Kulingana na watafiti hao, uhaba wa vifaa vya kupima virusi vya Corona pamoja na kuchelewa kupima kumesababisha kutokea kwa vifo kadhaa katika mataifa ya Italia na Uhispania, tofauti na Ujerumani ambako visa viligunduliwa mapema. Ujerumani imegundua takribani asilimia15% ya visa vyote ikilinganishwa na asilimia 3.5% na 1.7% ya visa ambavyo vimegundliwa Italia na Uhispania mtawalia, utafiti huo umebaini. Aidha unaeleza kuwa idadi ya visa vilivyogunduliwa nchini Marekani na Uingereza ilikuwa chini zaidi kwa asilimia 1.6% Marekani na huko Uingereza ikiwa tu kwa 1.2%
Suala la muda tu, kubainika hali mbaya nyingine
Watafiti hao (Christian Bommer na Sebastian Vollmer) wametoa wito kwa mataifa kuongeza juhudi za kupima na kugunduwa maambukizi mapya mapema pamoja na kuchukua mikakati ikiwemo kuwatenga waathirika ku. "Ikiwa mataifa yatashindwa kufanya hivyo, huenda virusi hivyo vikabaki bila kugunduliwa na kuweza kusababisha mripuko mwingine, ni suala la muda tu." Watafiti hao wametahadharisha.
Chanzo: AP