1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utafiti: Sera ya wakimbizi ilivyoibadili Ujerumani

24 Agosti 2016

"Tunamudu hilo", alidai Kansela Angela Merkel mwaka mmoja uliopita. Je, alikuwa sahihi au Ujerumani imekwenda mbali kwa kuwapokea wakimbizi zaidi ya milioni moja? DW iliwauliza raia kuhusu mtazamo wao.

Deutschland Flüchtling macht Selfie mit Merkel in Berlin-Spandau
Picha: Reuters/F. Bensch

Ni taswira zilizojaa ishara: Wanaume, wanawake na watoto, wengi wao kutoka Syria, Afghanistan na Iraq wakitembea kuelekea kaskazini katika misururu isioisha kwenye kile kinachojulikana kama njia ya Balkan.

Mamia kwa maelfu ya wahamiaji waliwasili Ujerumani mwanzoni mwa majira ya kiangazi mwaka 2015. "Tunaweza kulimudu hilo," alisema Kansela Angela Merkekl mjini Berlin Agosti 31. Ni maneno yalioongoza sera yake ya milango wazi kuhusu uhamiaji.

Je, sera hii imeibadili Ujerumani, na ikiwa ndiyo, kivipi? DW iliiagiza kampuni ya utafiti wa maoni ya Infratest Dimap kuwauliza raia maoni yao. Uchunguzi huu wa maoni ulitaka kupata mtazamo wa karibu wapigakura 1000 waliosajiliwa katika kipindi cha kuanzia Agosti 15 hadi 17.

Washiriki walipewa matamko manne kuhusu matokeo ya sera ya uhamiaji na kuulizwa iwapo wanakubaliana au la na matamko hayo.

Elimu na masuala ya kijamii

Gharama zinazohusiana na kuwasaidia wahamiaji zinakadiriwa kuwa siyo chini ya euro bilioni 15 kila mwaka. Wale waliowasili kwanza wanapaswa kupewa nyumba na chakula. Ujumuishwaji unawezekana tu ikiwa watu wanajifunza Kijerumani na wana elimu. Waalimu wanahitajika kwa ajili ya hili, na vilevile kwa ajili ya elimu na huduma kwa watoto katika vituo vya kuhuduma za mchana na shule. Je, hii itaiongezea mzigo mifumo ya elimu na kijamii ya Ujerumani? Ndiyo, ulisema mwingi mdogo wa walioulizwa.

Wafuasi wa Chama Mbadala kwa Ujerumani AfD wanapinga kabisaa sera ya Merkel ya uhamiaji.Picha: Getty Images/A. Hassenstein

Mfumo uliozidiwa wa elimu na kijamii ni hofu walionayo hasa wafuasi wa chama cha itikadi kali za mrengo wa kulia cha Alternative für Deutschland AfD. Ni asilimia 15 tu ya wafuasi wa AfD walioshiriki uchunguzi huu, ndiyo hawakukubaliana na tamko hili.

Madhara ya kiuchumi

Mtu anaeweza kuzungumza Kijerumani, ambaye ana elimu na uwezo wa kimwili, anapaswa kuwa na fursa ya kutafuta nafasi katika soko la ajira la Ujerumani. Ujerumani inakabiliwa na changamoto kubwa ya kidemografia. Watu wanazeeka na kuacha nguvukazi bila idadi kubwa ya vijana wenye nguvu kuwafuata. Hili linahisiwa hasa na makampuni. Kwa kila watu 100 wasio na ajira, kuna karibu nafasi 200 zilizowazi kwa watu watu wenye ujuzi. Je, wahamiaji na wakimbizi wanaweza kujaza nafasi hizi?

Kansela Merkel akitoa tamko la serikali mjini Berlin kuhusu sera ya wkimbizi bungeni Februari 17, 2016.Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Schreiber

Jibu la swali siyo jepesi sana. Nchini Ujerumani, nyanja za uhandisi wa ufundi, sekta ya magari na uhandisi wa umeme zinachangia asilimia 20 ya uzalishaji wa kiuchumi wa nchi. Sekta hizi hata hivyo, hazina uwakilishi katika mataifa asili ya wahamiaji. Kwa sababu hii, karibu wanakosa vigezo vinavyohitajika. Licha ya hayo, wingi mdogo wa washiriki wa uchunguzi huu walikuwa na maoni kwamba wafanyakazi wahamiaji watauimarisha uchumi wa Ujerumani.

Kama ilivyokuwa kwa maswali kuhusu elimu na mfumo wa kijamii, wafuasi wa chama cha AfD hawaoni manufaa yoyote kwa soko la ajira kutokana na kuwasili kwa wahamiaji. Tisa kati ya wafuasi wa AfD walikuwa na mtazamo huu. Lakini katika kujitenga na mapendeleo ya kisiasa, Wajerumani vijana na wale wenye elimu ya juu au wenye kipato cha juu walikuwa na mtazamo kwamba wakimbizi watauimarisha uchumi wa Ujerumani. Wale walio na miaka zaidi ya 50 na wale wenye elimu ya msingi hawakubaliani na hoja hiyo.

Ujerumani inazidi kutokuwa ya Wajerumani?

Kuwasili kwa wakimbizi si tu kuna madhara kwa uchumi, lakini pia kwa jamii kwa ujumla. Ujerumani tayari ni nyumbani kwa watu wengi wenye asili ya kigeni, hususani katika miji mikubwa. Kuna uwezekano wa hali hii kuzidi huko mbeleni. Je Wajerumani wanafikiria nini juu ya hili?

Hata hapa uhusiano wa kisiasa unatoa mchango, ambapo Wajerumani vijana na wasomi wana uwezekano mkubwa wa kukubali jamii yenye utamaduni mchanganyiko. Pia hawa wanapinga kwa nguvu kuhusishwa sera ya uhamiaji ya kansela Merkel na kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi. Wakati huo, wazee na walio na elimu ndogo wanakubaliana na mtazamo kwamba Ujerumani itakabiliwa na mashambulizi zaidi ya kigaidi katika siku zijazo.

Uturuki ndiyo inaongoza kwa kuwapokea wakimbi wa Syria, ikiw ana zaidi ya milioni 2.5.Picha: picture-alliance/AP Photo/L. Pitarakis

Ugaidi zaidi wa makundi ya Kiislamu mbeleni?

Lakini uhusiano wa kisiasa unasababisha mgawiko linapokuja swali kuhusu ugaidi. Ni asilimia 7 tu ya wafuasi wa AfD waliokuwa na maoni kwamba hakutakuwa tena na mashambulizi ya kigaidi nchini Ujerumani katika siku zijazo.

Matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa Wajerumani wana maoni tofauti kuhusu seraya uhamiaji ya Merkel. Kuna urari kati ya uzito na udhaifu wa sera hiyo.

Kilicho tofauti ni wafuasi wa vyama vya Kijani na AfD. Idadi kubwa kabisaa wa wafuasi wa chama cha AfD wana mtazamo kwamba sera ya uhamiaji ya serikali itakuwa na athari hasi kwa Ujerumani bila kuchagua. Kwa upande mwingine, karibu theluthi tatu ya wafuasi wa chama cha kijani wanaamini nchi itavuka changamoto na kunufaika kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi iliowapokea.

Mwandishi: Chloe/Sabine Kinkartz

Tanfiri: Iddi Ssessanga

Mhariri:

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW