1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ongezeko la joto duniani linaongezeka kwa kasi kubwa

5 Juni 2024

Wanasayansi 50 wakuu wametahadharisha kuwa ongezeko la joto duniani linazidi kwa kasi "kubwa" wakati ambapo nafasi ya kuzuia kupanda kwa joto ndani ya malengo ya viwango vya kimataifa vilivyowekwa, ikiwa inafikia mwisho.

Picha ya ishara ya moshi kutoka katika bomba la moshi kwa uchavizi wa  anga uchafuzi wa hewa
Picha ya ishara ya moshi kutoka katika bomba la moshi kwa uchafuzi wa anga uchafuzi.Picha: Pond5 Images/IMAGO

Paris

 

Katika utafiti uliochapishwa leo katika jarida la Earth System Data, wanasayansi hao wanasema kwa wastani wa mwongo mmoja, nyuzi joto zimepanda kwa nyuzi 0.26 kutoka mwaka 2014 hadi 2023. Utafiti huu umekuja wakati ambapo wanadiplomasia kutoka kote duniani wanakutana nchini Ujerumani wiki hii kwa mazungumzo ya katikati ya mwaka ya tabi nchi, kuelekea Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa COP29 utakaofanyika Baku, Azerbaijan mwezi Novemba. Utafiti huu pia ni sehemu ya msururu wa ukaguzi wa tabia nchi uliowekwa kwa ajili ya kuziba mapengo yaliyopo kati ya ripoti za Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusiana na Tabia Nchi, IPCC ambazo zimekuw azikitolewa kwa wastani kila baada ya miaka sita, tangu mwaka 1988.