SiasaGabon
Gabon: Utawala wa kijeshi wamemteua Waziri Mkuu wa mpito
8 Septemba 2023Matangazo
Uteuzi huo ulifanyika hapo jana Alhamisi na ulitangazwa kwenye televisheni ya taifa. Sima, mwanauchumi mwenye umri wa miaka 68, alikuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Ali Bongo aliyeondolewa madarakani na maafisa wa kijeshi mnamo Agosti 30.
Aliwahi kuwa waziri mkuu wa Bongo kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2014. Alijiuzulu mwaka 2014 na kugombea urais 2016 na kwa mara nyingine tena mwaka huu chama chake kilikuwa sehemu ya muungano wa upinzani.
Kiongozi wa kijeshi wa Gabon jenerali Brice Oligui Nguema ameahidi kuleta mageuzi ya kiuchumi na amesema ataandaa uchaguzi huru na wa haki, ingawa hajasema ni lini uchaguzi huo utafanyika.