Utawala wa kijeshi Guinea waamuru kuvunjwa kwa serikali
20 Februari 2024Matangazo
Hayo yameelezwa na msemaji wa utawala huo wa kijeshi Jenerali Amara Camara bila hata hivyo kutoa sababu za uamuzi huo wala kusema ni lini serikali mpya itakapotangazwa.
Jenerali Camara ameongeza kuwa kwa sasa shughuli za serikali zitasimamiwa na wakurugenzi wa baraza la mawaziri, makatibu wakuu na manaibu katibu hadi serikali mpya itakapoteuliwa. Guinea imekuwa ikiongozwa na jeshi tangu mapinduzi ya mwezi Septemba mwaka 2021.
Kiongozi wa zamani wa Kijeshi wa Guinea atoroshwa gerezani
Kufuatia shinikizo la kimataifa, kiongozi wa serikali hiyo ya kijeshi Kanali Mamady Doumbouya ameahidi kufanya mageuzi makubwa nchini humo na pia kuwa atarejesha utawala kwa viongozi wa kiraia watakaochaguliwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.