1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuinea

Utawala wa kijeshi Guinea wamteua Oury Bah kuwa Waziri Mkuu

28 Februari 2024

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umemteua waziri mkuu mpya siku nane tu baada ya kuivunja serikali wakati shughuli katika mji mkuu wa Conakry zimesimama kufuatia siku ya pili ya mgomo wa kitaifa wa wafanyikazi.

Kiongozi wa utawala wa kijeshi wa Guinea Kanali Mamady Doumbouya
Kiongozi wa utawala wa kijeshi wa Guinea Kanali Mamady DoumbouyaPicha: uncredited/AP/picture alliance

Katika hotuba ya televisheni, msemaji wa utawala huo wa kijeshi unaoongozwa na Kanali Mamady Doumbouya amesema Amadou Oury Bah, mchumi na aliyekuwa wakati mmoja kiongozi wa upinzani, ameteuliwa kuhudumu kama waziri mkuu na mkuu wa serikali.

Doumbouya ameongeza kuwa waziri mkuu huyo mpya atapewa jukumu la kushughulikia mvutano na vyama 13 vya wafanyikazi vilivyoitisha mgomo wa kitaifa ulioanza siku ya Jumatatu.

Soma pia:  Idadi ya waliokufa kutokana na moto Guinea yafikia 23

Vyama vya wafanyikazi vinashinikiza kuachiliwa huru kwa katibu mkuu wa muungano wa wanahabari wa Guinea Sekou Jamal Pendessa, kushuka kwa bei ya vyakula, kuondolewa kwa udhibiti wa vyombo vya habari na mtandao wa intaneti pamoja na kutimizwa ahadi ya nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma.

Shule, maduka, masoko na barabara katika mji mkuu Conakry zimesalia tupu huku hospitali zikitoa huduma ndogo ndogo pekee.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW