Myanamar na Urusi zashirikiana kuhusu shughuli za uchaguzi
13 Septemba 2023Taarifa zilizotolewa leo na gazeti la serikali nchini Myanmar zimesema maafisa wa tume ya uchaguzi iliyowekwa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo wamesaini mkataba wa maelewano ya ushirikiano wa shughuli za uchaguzi na wenzao wa Urusi wakati wa ziara walioifanya hivi karibuni nchini Urusi.
Marekani kuishinikiza Myanmar kufuata njia ya demokrasia
Ujumbe huo wa Myanmar pia ulijifunza kuhusu njia zinazotumiwa katika uchaguzi nchini Urusi,mazingira ya kufanya chaguzi pamoja na michakato ya kampeini.
Nchi zote hizo mbili zinajiandaa kwa chaguzi ambazo wakosoaji wanasema hazitokuwa huru wala hazitozingatia haki.
Jeshi la Myanmar lilihalalisha mapinduzi yake kwa kudai kwamba uchaguzi wa mwaka 2020 uliompa ushindi Aung San Suu Kyi na chama chake kinachopigania demokrasia,NLD, uligubikwa na udanganyifu mkubwa.