1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Utawala wa Myanmar wathibitisha kushambulia kijiji

12 Aprili 2023

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar leo umethibitsha kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya kijiji cha Kanbalu katika eneo la Kati la Sagain nchini humo ambapo watu kadhaa wameripotiwa kuuawa.

Kijiji kilichoshambuliwa Myanmar
Tangu jeshi lilipochukua madaraka kwa nguvu nchini Myanmar Februari 2021, mashambulizi ya anga dhidi ya vijiji hutokea kila wakati.Picha: Kyunhla Activists Group/AP/picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Idadi ya waliofariki kutokana na shambulizi hilo la mapema jana bado haijajulikana.

Hata hivyo takriban vifo 50 na kujeruhiwa kwa watu wengine wengi kumeropitiwa na shirika la BBC la Burma, shirika la Irrawaddy na Radio Free Asia, pamoja na shahidi aliyewasiliana na shirika la habari la AFP.

AFP imeripoti kuwa ndege za kijeshi zilivamia kijiji cha Pazi Gyi ambapo wakazi walikuwa wamekusanyika kuadhimisha kufunguliwa kwa ofisi ya kikosi cha ulinzi wa eneo hilo, kinachoshirikiana na wapinzani wa jeshi hilo.

Jeshi hilo lilithibitisha kufanya mashambulizi hayo baada ya kupata fununu kuhusu hafla hiyo.

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuadhibishwa kwa wale waliohusika katika shambulizi hilo.