1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger yatengua sheria ya kuwabana wanaokwenda Ulaya

28 Novemba 2023

Watawala wa kijeshi nchini Niger wameidhinisha amri ya kubatilisha sheria ya mwaka 2015 iliyotungwa kwa ajili ya kuzuia wimbi la wahamiaji wanaosafiri kutoka nchi za Kiafrika kwenda bara Ulaya kupitia nchini Niger.

Wajamiaji wakiwa katika ofisi ya Wahamiaji ya Umoja wa Mataifa IOM
Wajamiaji wakiwa katika ofisi ya Wahamiaji ya Umoja wa Mataifa IOMPicha: ANTHONY ANEX/KEYSTONE/picture alliance

Eneo la Agadez nchini humo ndio lango kuu linalotumiwa na Waafrika wanaojaribu kufika Libya ili kuvuka bahari ya Mediterania kwenda Ulaya na pia kwa watu wanaorudi nyumbani kwa msaada kutoka Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa serikali ya Niger, Jenerali Abdourahmane Tchiani, amesema hukumu zote zilizotolewa kwa mujibu wa sheria hiyo zitafutwa.

Kulingana na waraka huo uliotiwa saini tarehe 25 mwezi huu, katibu mkuu wa wizara ya sheria ya Niger Ibrahim Jean Etienne amesema watu wote waliopatikana na hatia chini ya sheria hiyo wataachiliwa.

Soma pia:Kiongozi wa kijeshi Niger afanya ziara Mali na Burkina Faso

Hatua ya kutengua sheria inaongeza mvutano kati ya Niger na nchi za Umoja wa Ulaya ambazo zililiwekea vikwazo taifa hilo la Afrika Magharibi.

Hatua hiyo ilikuwa ni majibu ya mapinduzi ya kijeshiya mwezi Julai yaliyomwondoa mamlaka Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kuwaweka watawala wa kijeshi madarakani.
 

Vuguvugu la wahamaji Kusini mwa Jangwa la Sahara

01:50

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW