1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utetezi wa Tutu wa mashoga haukuwashawishi Waafrika wengi

Hawa Bihoga
29 Desemba 2021

Desmond Tutu mbali na kukumbukwa katika kupigania haki za watu weusi, anakumbukwa pia kwa utetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja. Hata hivyo, kampeni yake haikuwa na matokeo makubwa katika maeneo mengi ya Afrika.

Südafrika Desmond Tutu
Picha: Nardus Engelbrecht/AP/picture alliance

Ndani ya dhehebu lake la Anglikana kwa bara zima la Afrika imekuwa ni marufuku kukumbatia haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ikipigiwa mfano viongozi wa Anglikana nchini Ghana walijiunga na viongozi wengine wa kidini katika kuidhinisha muswada ambao utatoa hukumu ya kwenda jela kwa watu watakaojitambulisha kuwa ni wapenzi wa jinsia moja au kuunga mkono kundi hilo.

Soma pia: Ta'azia: Askofu Mkuu Desmond Tutu, mwanaharakati asiyechoka

Mtafiti wa shirika la kutetea maslahi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja la Outright Action International nchini Kenya, Yvonne Wamari anasema kabla ya Tutu kufariki siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka tisini viongozi wengi wa kidini barani Afrika walipinga nafasi aliokuwa nayo katika jamii hiyo ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, hata wale ambao walikubaliana na misimamo yake mara zote walikuwa waangalifu. Wengi wao wamekuwa hawako tayari kutoa maoni yao wakihofia kwenda kinyume na maadili ya Kiafrika.

Maisha na urithi wa Askofu Desmond Tutu

03:58

This browser does not support the video element.

Wamari aliongeza kuwa viongozi wa dini waliochukua mrengo wa kukataa kutetea kundi hilo hawako tayari kutafsiri Biblia kutoka kwa mukhtadha wa upendo kwa wote, kama Tutu alivyofanya, chuki dhidi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na wale wanaopigania haki zao  itabaki kuwa sehemu yetu maisha. Masuala ya ushoga yamesalia kuwa ni marufuku kwa zaidi ya nchi 30 barani Afrika, machache kati ya hayo yamepitisha adhabu ya kifo kwa watakaobainika.

Kundi hilo kwa barani Afrika bado linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo unyanyapaa na unyanyasaji, ukosefu wa ajira, ukosefu wa makaazi na hata kutengwa na familia zao. Profesa  Stephen Brown wa Chuo Kikuu cha Ottawa alimtaja Tutu kama mtu mwenye maadili na  alieshikilia msimamo wake ikiwa ni pamoja na usaidizi kwa kundi hilo bila kujali hatari ya chuki inayoweza kuwa mbele yake.

Soma pia: Vifo vya watu maarufu vilivyotokea 2021

Mjini Cape Town, ambapo Tutu alikuwa askofu mkuu wa Kianglikana, washiriki wa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja ilipokea kifo chake kwa heshima. Daniel Jay, ambaye anafanya kazi katika sekta ya matibabu, amekiriwa akisema msaada wa Tutu kwa watu wa kundi hilo ilikuwa muhimu kwani alifanikiwa kuipambania Afrika Kusini kutoa dawa za VVU bila malipo kwa watu hao.

Nje ya mipaka ya Afrika Kusini kumeshuhudiwa maendeleo kwa kiasi fulani juu ya upatikanaji wa haki kwa kundi hilo, nchini Botswana, Mahakama ya Rufaa mwezi uliopita kwa kauli moja ilikubali uamuzi wa 2019 ulioharamisha shughuli za watu wa jinsia moja. Hapo awali, ngono ya mashoga ilipigwa marufuku na wahalifu walikabiliwa na hadi miaka saba jela, huku mataifa mengine kama vile Angola, Msumbiji na Ushelisheli yakichukua msimamo kama huo.

Desmond Tutu akiwa na rafiki yake, kiongozi wa kiroho na kisiasa wa Watibet, Dalai Lama.Picha: ANNA ZIEMINSKI/AFP

Nchini Namibia hivi karibuni ilifanyika sherehe kubwa iliopambwa kwa maandamano huko katika mji mkuu wa taifa hilo, Windhoek ambapo waandamanaji walihimiza kufutwa kwa sheria ya kupinga ulawiti ambayo kwa muda mrefu sasa haijatekelezwa, wakati huko nchini Ghana wabunge wanaendelea kuufanyia kazi muswada ambao unalaani vikali na kupiga marufuku watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Soma pia: Afrika Kusini imeanza wiki ya maombolezo

Tutu kila alipopata wasaa wa kuzungumzia mada hiyo alizungumza kuhusu jinsi watu wote wanavyokumbatiwa na Mungu, bila kujali jinsia au rangi huku akiwajumuisha mashoga na wasagaji katika orodha hiyo, hatua iliyoleta mshindo mkubwa, mshangao, utulivu na furaha miongoni mwa watu wa kundi hilo.

Chanzo: Associated Press

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW