1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utoshelevu wa chakula unatarajiwa kushuka

29 Novemba 2021

Wakati nchi ya Tanzania ikielekea katika maadhimisho ya miaka 60 tangu nchi hiyo ijipatie uhuru, yaelezwa kuwa hali ya utoshelevu wa chakula inatarajiwa kushuka kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Afrika Tansania Prof. Adolf Mkenda
Picha: Deo Kaji Makomba/DW

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa kilimo nchini Tanzania Profesa Adolf Mkenda, wakati akizungumza katika tathimini ya Wizara yake tangu nchi hiyo ijipatie uhuru. 

Akizungumza katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru mnamo Decemba 9 mwaka huu Waziri Profesa Mwaikenda amesema kuwa, utoshelevu huo wa chakula katika msimu huu utashuka hadi asilimia 107 kutoka asilimia 125 na hivyo kuwataka wananchi kulima mazao yanayostahillmili ukame. 

Amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wataalam wa kilimo kwa kushirikiana na wataalam wa mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania umebaini kuwa kuna baadhi ya maeneo nchini humo yatakabiliwa na changamoto kubwa ya ukame huku baadhi ya maeneo mengine yakiwa bado yana nafasi ya kuzalisha chakula cha ziada na kuongeza kuwa.

Ushauri kwa wakulima

Picha: CC/Anne Wangalachi/CIMMYT

"Baada ya kufanya utafiti huu, tumeanisha maeneo kwa Wilaya na sehemu nyingine ambazo zitakuwa na changamoto kubwa zaidi na kulifanyika mkutano wa Wakuu wa Mikoa wote wakapitishwa vizuri kila mkoa tunatarajia nini, na wenyewe wamelibeba wanapeka kule kwa ajili ya kuwasaidia wakulima hivyo nawaomba wakulima ushauri utakaokuwa unatolewa na viongozi wetu yale maeneo tumeshauri tulime mazao yanayositahimili ukame tuzingatie ili tuepuke kuja kuwa na changamoto kubwa ya chakula kutokana na hali ya hewa" alisema  Profesa Adolf Mwaikenda.

soma Tanzania yashikwa na hofu ya kukumbwa na ukame

Katika kukabiliana na changamoto hiyo serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya kilimo imesema itahakikisha inasimamia miradi ya kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wananchi katika maeneo yatakayokabiliwana na ukame kulima mazao yanayositahimili ukame ikiwemo mtama. 

Kauli hiyo ya Waziri wa kilimo nchini Tanzania imewaibua Wachambuzi wa masuala ya chakula Audax Rukonge, mkurugenzi wa shirika linalohusika na masuala ya kilimo nchini Tanzania.

"Katika hili tu naona kwamba upungufu wa chakula umetokana na ukosefu wa maji na hili lilitegemewa liwepo kwasababu toka mwezi wa tisa mamlaka ya hali ya hewa ilikwishatoa utabiri wa hali ya hewa na hasa hasa kwenye masuala ya mvua Kwahiyo tulitegemea sasa kama serikali wake na mpango na mfumo wa namna gani tunahamasisha upatikanaji wa Teknolojia ya kuvuna maji ya mvua kuyatunza na hayo maji yatumike kumwagilia ili miaka inayo kuja linapotokea tatizo kama ambalo tumeliona mwaka huu basi tuwe na maji ya kutosha" Alisema Audax Rukonge.

Katika msimu uliopita wa mavuno Tanzania ikijipatia mavuno mengi ya chakula ikiwemo mahindi hadi kufikia wakulima kulalamika ukosefu wa masoko ya mazao yao. 

 

Deo Kaji Makomba/DW

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW