Utulivu warejea Nepal
11 Septemba 2025
Wawakilishi wa waandamanaji wanafanya mazungumzo na viongozi wa jeshi kwenye makao makuu ya jeshi mjini Kathmandu kwa lengo la kumpata kiongozi wa mpito.
Baadhi ya waandamanaji wanampendekeza jaji mkuu wa zamani, Sushila Karki, kuchukuwa nafasi hiyo.
Karki ndiye mwanamke pekee kuwahi kushikilia wadhifa wa jaji mkuu kwenye taifa hilo la Asia.
Uamuzi wa serikali kutumia vyombo vya usalama vilivyowauwa watu 19 kuzuwia maandamano ya Jumatatu yaliyoitishwa na vijana kupinga amri ya kupiga marufuku mitandao ya kijamii, ulizusha hasira kubwa ya umma.
Maelfu ya raia walijitokeza mitaani kuishinikiza serikali na kupelekea Waziri Mkuu Khadga Prasad Oli kujiuzulu na kukimbia.
Hatima ya alipo Oli haijafahamika hadi sasa.
Wizara ya Afya ya Nepal ilisema idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye maandamano hayo imefikia 25.