Utumwa mambo leo katika ajira
17 Agosti 2016Kulingana na ripoti mpya iliyotolewa hivi karibuni kuhusu viwango vya kutumikishwa watu katika ajira, Korea Kaskazini ndiyo nchi iliyo na rekodi mbaya zaidi ya kutumikisha watu katika ajira.
Utafiti uliofanywa na kampuni ya Verisk Maplecroft ikitumia vigezo vya visa vilivyoripotiwa vya usafirishaji watu kwa njia zisizo halali au utumwaDRC, sheria za nchi na utendaji wa vyombo vya dola katika nchi 198, kampuni hiyo imegundua kuwa nchi 115 ziko katika hatari ya kuwatumia watumwa.
Mtafiti mkuu wa kampuni hiyo aliyeongoza ukusanyaji wa data kuhusu haki za binadamu Alex Channer amesema ni nchi chache duniani ambazo haziko katika hatari ya kutumia utumwa mambo leo.
Ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu duniani la Walk Free inasema takriban watu milioni 46 duniani wanaishi kama watumwa, wakilazimishwa kufanya kazi katika viwnada, migondini na katika mashamba wakiuzwa kama watumwa wa ngono au kuzaliwa utumwani.
Utumwa mambo leo unabainika katika baishara haramu ya kuwasafirisha watu, kuwatumikisha katika ajira, kuwafunga katika lindi la madeni, ndoa za lazima, utumikishwaji kingono, kuwa chini ya mtu ambae anamtawala na madhila mengineyo.
Mataifa mbalimbali yanafanya juhudi kukomesha tatizo hilo. Mwaka uliopita Uingereza ilipitisha sheria ya kupinga utumikishaji wa watu, ikizitaka kampuni kubwa zinazopata faida ya zaidi ya Pauni milioni 36 au zaidi kuripoti zinachukua hatua gani kukomesha utumwa katika uzalishaji wao wa bidhaa
Sudan Kusini na DRC zatajwa kuwa na kiwango cha juu
Mbali na Korea Kaskazini, ripoti hiyo inataja mataifa mengine yanaoongoza katika biashara haramu na utumikishaji kuwa ni pamoja na Sudan Kusini, Jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo DRC, taifa ambalo ndilo mzalishaji mkubwa duniani wa madini ya Cobalt yanayotumika katika kutengeneza vifaa vya elektroniki.
Katika kusafiririsha vifaa vizito China na India zinaongoza ikiwa ni pamoja na nchi za DRC, Ivory Coast ambayo Inaongoza katika uzalishaji wa Kakao.
Nchi za Umoja wa Ulaya zinatajwa kuwahi kuwa na kiwango cha wastani cha utumikishaji watu, Hata hivyo mataifa manne tu Ujerumani, Uingereza, Dernmak na Finland yanatajwa kuwa na kiwango cha chini cha kuwatumikisha watu katika ajira.
Utafiti huo kuhusu viwango vya utumwa mambo leo na kuzitaja nchi zilizo katika hatari ya kutumikisha watu,unalenga kuzisaidia biashara duninai kugundua nchi ambazo huenda zitakutimia watumwa mambo leo katika uzalishaji wa bidhaa zao.
Suala hilo la utumikishaji limeangaziwa pakubwa katika miaka ya hivi karibuni hasa katika sekta za uvuvi, madini na katika viwanda vya kutengeneza nguo.
Mwandishi: Celina Mwakabwale/Reutes
Mhariri: Caro Robi