1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Uturuki yadai kuwauwa wapiganaji wengi wa PKK

2 Oktoba 2023

Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema mashambulizi ya angani yaliyofanywa na nchi hiyo yamewasambaratisha wanamgambo wa kikurdi na kuharibu maghala yao na makaazi yao Kaskazini mwa Iraq.

Mwanajeshi wa Uturuki akiwa kwenye Mlima Balkaya ambako kuna kambi iliyojengwa mahususi ili akifuatilia shughuli za wanamgambo wa PKK
Mwanajeshi wa Uturuki akiwa kwenye Mlima Balkaya ambako kuna kambi iliyojengwa mahususi ili akifuatilia shughuli za wanamgambo wa PKKPicha: Ozkan Bilgin/AA/picture alliance

Operesheni hiyo ya jeshi la Uturuki ilifanyika katika maeneo ya Metina, Hakurk, Qandil na Gara kaskazini mwa Iraq. Wizara hiyo imesema hatua za tahadhari zilichukuliwa kuepuka madhara kwa raia na mazingira.

Wizara hiyo imetoa tamko hilo saa kadhaa baada ya chama cha jamii ya kikurdi cha PKK kukiri kuhusika na shambulio la bomu mjini Ankara.

Mshambualiaji mmoja alijiripua karibu na majengo mawili ya serikali mjinii humo jana asubuhi na kusababisha maafisa wawili wa polisi kujeruhiwa. Mwenzake mwingine aliyekuwa pia na mkanda wa mabomu alipigwa risasi na kuuwawa kabla ya kujiripua.

Chama cha PKK kimeorodheshwa kama kundi la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya.