SiasaUturuki
Uturuki inaamua kati ya Erdogan au Kiliçdaroglu
28 Mei 2023Matangazo
Karibu wapiga kura milioni 61 wanashiriki uchaguzi huo unaofanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi majira ya saa kumi na moja jioni kwa saa za Uturuki.
Uchaguzi wa leo unafanyika baada ya duru ya kwanza kushindwa kutoa mshindi wa wazi kati ya rais aliye madarakani anayewania muhula mwingine Recep Tayyip Erdogan dhidi ya mpinzani wake mkuu Kemal Kiliçdaroglu.
Kura ya leo inatajwa kuwa kipimo cha utawala wa miongo miwili ya Erdogan anayetuhumiwa na upinzani kwa sera za "mabavu".
Uchaguzi huo unafanyika ikiwa imepita miezi mitatu tangu kutokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki lililowaua maelfu ya watu na katikati ya mdodoro mkubwa wa kiuchumi kuwahi kushuhudiwa nchini humo.