1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUturuki

Uturuki kujiunga kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel

7 Agosti 2024

Uturuki itawasilisha maombi kwenye mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kujiunga katika kuishtaki Israel kwa mauaji ya kimbari.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.Picha: Marko Djurica/REUTERS

Mashtaka hayo yaliwasilishwa na Afrika Kusini. Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizojiunga hivi karibuni ili kushiriki katika kesi hiyo.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan mara kwa mara ametoa miito ya kutaka Israel iadhibiwe na mahakama za kimataifa na amezikosoa nchi za Magharibi kwa kuiunga mkono Israel.

Mnamo mwezi wa Mei Uturuki ilisimamisha shughuli za kibiashara na Israel.

Afrika Kusini iliwasilisha kesi hiyo kwenye Mahakama ya Haki ya Umoja wa Mataifa, ICJ mwaka uliopita kwa kuilaumu Israel kwa kukiuka mkataba wa kuzuia mauaji ya halaiki, kutokana na operesheni zake za kijeshi kwenye Ukanda wa Gaza.

Hata hivyo, Israel imeyakanusha vikali madai hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW