1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki kutuma vikosi vya jeshi Libya

Sekione Kitojo
27 Desemba 2019

 Uturuki itapeleka vikosi vya jeshi lake nchini Libya kwa ombi la serikali ya mjini Tripoli mwezi ujao, amesema rais Tayyip Erdogan jana, akiuweka mzozo wa nchi hiyo ya Afrika kaskazini katika msuguano zaidi wa kikanda.

Türkei Istanbul | Libyens Premierminister al-Sarraj trifft Erdogan
Picha: picture-alliance/AP Photo/Turkish Presidency

Waziri mkuu  wa  Italia  Giuseppe Conte na  rais wa  Urusi  Vladimir Putin  hata  hivyo  wametoa wito wa kupatikana suluhisho  la  mzozo  huo  kwa  njia  ya  amani.

Wapiganaji wa serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli wakiwa katika doria mjini TripoliPicha: picture-alliance/Photoshot/H. Turkia

Serikali ya  Libya  inayotambulika kimataifa  serikali ya  maridhiano ya  kitaifa GNA mjini  Tripoli imekuwa  ikihangaika  kuzuwia  majeshi ya  mbabe  wa  kivita  jenerali Khalifa  Haftar, ambayo  yamekuwa yakiungwa  mkono  na  Urusi, Misri, Umoja  wa  falme za  Kiarbu UAE  na  Jordan.

Afisa  mjini  Tripoli amethibitisha  kutolewa ombi  rasmi kwa  msaada wa  majeshi  ya  Uturuki  angani, ardhini  na  baharini.

Afisa  huyo , ambaye  hakutaka  kutajwa  jina , amezungumza baada ya  waziri  wa   mambo  ya  ndani  wa  serikali  ya  mjini  Tripoli, Fathi Bashagha , kuashiria  katika  maelezo  kwa  waandishi  habari  mjini Tunis  kuwa  hakuna  ombi  kama  hilo lililotolewa.

" Serikali ya maridhiano  ya  kitaifa  imetia  saini  taarifa ya makubaliano na  serikali ya  Uturuki  chini  ya  msingi  wa  ombi kutoka  Uturuki. Tunaamini  kuwa  kutakuwa  na  ushirikiano  mkubwa na  Uturuki, Tunisia, na  Algeria, na  tutakuwa  katika  ushirika  katika njia  kwamba  unawanufaisha  watu  wetu na uthabiti  wa  usalama wetu, pamoja  na  uchumi  ambao  ni chanzo cha  wasi  wasi  kwetu sote. ushirikiano  wa  kiuchumi unahitaji  uthabiti  katika  usalama pamoja  na  uthabiti wa  kisiasa."

Wapiganaji watiifu kwa mbabe wa kivita Khalifa HaftarPicha: Getty Images/AFP/A. Doma

Marekani afanya mazungumzo na  Sisi

Majeshi  ya  Haftar yameshindwa  kufika  katikati  ya  Tripoli  lakini yamepata  mafanikio  madogo  katika  wiki  za  hivi  karibuni  katika baadhi  ya  maeneo  ya  nje  ya  mji  huo  upande  wa  kusini kwa msaada  wa  wapiganaji  kutoka  Urusi  na  Sudan, pamoja  na ndege  zisizo  na  rubani  zilizoingizwa  na  Umoja  wa  Falme za kiarabu, UAE, wanadiploamsia  wamesema.

Rais wa  Marekani Donald Trump jana  alifanya  mazungumzo  ya simu  na  rais  wa  Misri  Abdel Fattah al-Sisi, ikulu  ya  Marekani  ya White House  imesema, ambapo  viongozi hao  wawili walikataa  kile walichosema  kuwa  ni  mataifa  ya  nje  kuitumia  Libya.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-SisiPicha: picture-alliance/AFP/J. Macdougall

Uturuki  tayari  imekwisha  tuma  vifaa  vya  kijeshi  kwa  serikali hiyo maridhiano ya  kitaifa licha  ya  vikwazo  vya  silaha  vya  Umoja  wa mataifa  kwa  Libya , kwa  mujibu  wa  ripoti ya  Umoja  wa  mataifa iliyopatikana  na  shirika  la  habari  la  Reuters mwezi  uliopita.

Rais  wa  Urusi Vladimir  Putin  na  waziri  mkuu  wa  Italia Giuseppe Conte walikubaliana  jana  kuwa  hali  nchini  Libya  inapaswa kutatuliwa  kwa  njia  ya  amani, ikulu  ya  urusi  Kremlin imesema.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW