Uturuki-Syria: Idadi ya vifo yaongezeka na kufikia 28,000
12 Februari 2023Matangazo
Shirika la utangazaji la serikali ya Uturuki TRT, limetangaza leo kuwa mtoto wa miezi 7 ameokolewa akiwa hai kusini-mashariki katika jimbo la Hatay baada ya kukaa masaa 140 chini ya vifusi.
Mtaalamu wa Ujerumani na mfanyakazi wa shirika la misaada la NAVIS Thomas Geiner, ameonya juu ya hatari ya kutokea milipuko ya magonjwa kutokana na uhaba wa maji safi na miundombinu muhimu kama choo huku akitoa wito wa kupatikana misaada kwa haraka.