Uturuki yaambiwa na Bush iondoke kaskazini mwa Irak
29 Februari 2008Matangazo
WASHINGTON:
Rais George W.Bush wa Marekani ameitaka Uturuki iondoshe vikosi vyake kutoka kaskazini mwa Irak upesi iwezekanavyo.Hapo awali Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates alipokutana na maafisa wa Uturuki mjini Ankara alisema;hatua za kijeshi pekee hazitomaliza mzozo wa Uturuki na Wakurdi wa chama cha PKK. Akatoa mwito kwa serikali ya Uturuki kuwasaidia Wakurdi walio wachache nchini humo.Juma moja lililopita,majeshi ya Uturuki yalivuka mpaka na kuingia kaskazini mwa Irak kuteketeza ngome za wanamgambo wa PKK katika eneo hilo.Serikali mjini Ankara inasema,waasi wa PKK wanatumia sehemu hiyo ya milimani kama kituo cha kufanya mashambulizi yake dhidi ya raia na wanajeshi ndani ya ardhi ya Uturuki.