1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yaanzisha upya mashambulio ya angani dhidi ya PKK

27 Julai 2008

-

ANKARA

Uturuki imeanzisha tena hii leo mashambulio ya angani dhidi ya maeneo ya waasi wa kikurdi wa chama cha PKK ndani ya ardhi ya kaskazini mwa Iraq.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jeshi la Uturuki,wamelenga mashambulio yao katika eneo la milimani la Kandil ambako ni waasi wa PKK wanamakao makuu yao.

Hata hivyo hakuna taarifa juu ya waliouwawa au kujeruhiwa kufuatia mashambulio hayo ya angani.

Ndege za kijeshi za Uturuki zimekuwa zikishambulia kwa mabomu maeneo ya waasi wa Kikurdi wa chama cha PKK kaskazini mwa Iraq tangu desemba mwaka jana.