1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yachagua rais mpya

Maja Dreyer25 Aprili 2007

Suala la kwanza ni Uturuki: Rais mpya wa Uturuki ataapishwa wiki nne zijazo, na jina lake huenda likawa Abdullah Gül. Huyu ni mgombea wa chama tawala cha waziri mkuu Erdogan ambaye mwenyewe ameamua kutogombea kiti cha rais.

Kuhusu hatua hiyo, gazeti la “Die Welt” limeandika:

“Bila shaka haikuwa rahisi kwake waziri mkuu Tayyip Erdogan kujihini, na kumpa fursa waziri wa mambo ya nchi za nje, Abdullah Gül. Kwa nchi za Ulaya, Gül ni chaguo zuri kwa sababu Gül kama waziri wa nje wa Uturuki amejipatia heshima. Pamoja na waziri mkuu Erdogan katika serikali ya Uturuki, Gül ataendelea na sera za nchi yake kukaribia Ulaya.”

Ni mtazamo kuhusiana na sera kuelekea Umoja wa Ulaya. Ndani ya Uturuki lakini kuna wasiwasi kwamba chama tawala cha AKP kina lengo la kuimarisha Uislamu nchini Uturuki, kwa sababu Gül anajulikana alikuwa na msimamo mkali wa kiislamu. Kwa hivyo gazeti la “Rheinische Post” linachambua ikiwa mkakati huo wa waziri mkuu Tayyip Erdogan wa kumteua Gül kweli unweza kufanikiwa?:

“Erdogan anajua kuwa licha ya kuwa na wingi katika bunge, yeye mwenyewe hawezi kuwa rais bila ya kukubaliwa na jeshi. Vilevile Erdogan aliona mamia ya Waturuki walioandamana dhidi yake kugombea kiti cha rais. Kwa hivyo inaonekana kuwa ni hatua busara kumteua waziri wa nje, Abdullah Gül. Lakini hilo si suluhisho, kwani Gül alikuwa mwanachama wa vyama viwili ambavyo hivi sasa vimepigwa marufuku.”

Uturuki, basi chini ya rais Gül itakuaje?

“Chama cha kihadifhina na cha kiislamu, pamoja na kudhibiti bunge na serikali, hivi karibuni itadhibiti pia ikulu.” Ni utabiri wake mhariri wa “Rhein-Zeitung”. Anaendelea kuandika:

“Ni jeshi tu pekee ambalo haliunganishi siasa na dini. Nchi za Ulaya zitakuwa na uangalifu zaidi. Demokrasia katika nchi ya Uislamu itakaribishwa, lakini udikteta wa kidini hautakubaliwa.”

Na kwa hapo tuangalie suala lingine ambalo lilizingatiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, yaani ripoti ya mwakilishi maalum wa serikali ya Ujerumani kwa suala la ulinzi wa taarifa zinazohusu watu binfasi zisitumiwe vibaya. Ni ripoti ya kusikitisha. Kwa mujibu wa gazeti la “Ostthüringer Zeitung” matumizi mabaya ya taarifa za watu yaliongezeka sambamba na kupatikana kwa teknolojia mpya. Limeandika:

“Habari mbaya zaidi katika ripoti ya mwakilishi huyu ni pale anaposema kuwa, kiteknolojia inawezekana kumdhibiti raia kila pahali. Na kile kinachowezekana huwa kinafanyika. Au tuseme, hatari ni kubwa.”

Na juu ya suala hilo hilo, gazeti la “Neue Presse “ la mjini Hanover limeandika yafuatayo:

“Tuko njiani kudhibiti kila kitu. Hadi sasa watu wachache tu walijihusisha na tatizo hili. Lakini ongezeko la taarifa za watu binafsi zinazokusanywa lilimpatia uangalifu mwakilishi maalum katika wizara ya mambo ya ndani na ripoti yake. Ingepaswa lakini, waziri mwenyewe afahamu kuwa ulinzi wa taarifa hizo ndio jukumu lake. “

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW