Uturuki yakubali kuiunga mkono Sweden kujiunga NATO
11 Julai 2023Matangazo
Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ambaye alikutana kwa mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Waziri Mkuu Ulf Kristersson wa Sweden mjini Vilnius, Lithuania, kunakoanza mkutano wa kilele wa siku mbili wa NATO.
Soma zaidi: Erdogan aondoa pingamizi kwa Sweden kujiunga na NATO
Mkutano wa NATO kuanza Jumanne nchini Lithuania
Hata hivyo, taarifa ya pamoja iliyotolewa na viongozi hao watatu haijabainisha ni kwa muda gani bunge la Uturuki litalazimika kuidhinisha ombi hilo la Sweden.
"Kukamilisha ombi la Sweden ni hatua ya kihistoria inayonufaisha usalama wa washirika wote wa NATO hasa katika wakati huu muhimu," alisema Stoltenberg.