Uturuki yaomboleza mauaji ya uwanja wa ndege
29 Juni 2016Serikali ya Uturuki imeamuru bendera kupepea nusu mlingoti.Hapo mwaka jana serikali ilitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya miripuko miwili ya kujitolea muhanga kuuwa zaidi ya watu 100 katika mji mkuu wa Uturuki Ankara hapo mwezi wa Oktoba shambulio ambalo pia linadaiwa kufanywa na kundi la Dola la Kiislamu.
Uwanja wa ndege huo wa Atartak mojawapo ya uwanja wa ndege mkubwa kabisa katika kanda ulifungwa kwa msaa kadhaa baada ya shambulio hilo la kinyama. Ndege zilianza tena kutuwa kabla ya alfajiri leo hii na ndege za kwanza zilianza kuondoka asubuhi wakati uwanja wa ndege huo ukianza shughuli zake kwa kiasi fulani.
Ali Batur aliyempoteza kaka yake katika shambulio hilo amesema "Tufikirie nini ?Hatuwezi kufikiria chochote.Shambulio la kigaidi linaweza kutokea popote pale huwa linatokea kila mahala.Tatizo la ugaidi pia lipo katika nchi yetu.Mungu akijaalia haya tutayamaliza kwa kuwa na umoja na mshikamano."
Ushirikiano wa kimataifa dhidi ya ugaidi
Umoja wa kitaifa na ushirikiano wa dunia ndio wito ulitolewa na Waziri Mkuu wa Uturuki Benali Yidrim katika kupambana na ugaidi.
Amesema shambulio hilo kwa mara nyengine limeonyesha kwamba ugaidi ni tatizo la dunia na kudokeza kwamba linahusiana na kile alichokisema mafanikio ya Uturuki dhidi waasi wa Kikurdi halikadhalika hatua ilizochukuwa nchi hiyo hapo Jumatatu kurekebisha uhusiano wake na Israel na Urusi.
Wakati Yildrim akisema uchunguzi unaashiria kuhusika kwa kundi la Dola la Kiislamu katika shambulio hilo hakuna ishara kwamba kuna washambuliaji wengine waliofanikiwa kukimbia.Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo
Marekani ilitowa onyo la vitisho kwa Uturuki
Hapo Jumatatu wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitowa oyno la kuongezeka vitisho dhidi ya Uturuki nchi mwanachama mwenzake katika Jumuiya Kujihami ya NATO. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amelilaani shambulio hilo la uwanja wa ndege wa Istanbul.
Kerry amesema "Bado tunaendelea kukusanya taarifa na kujaribu kuyakinisha kile kilichotokea na nani aliefanya hayo na hatutoweza kuzunngumzia zaidi juu ya jambo hilo isipokuwa tu kwa kusema changamoto ya kwanza inyotubidi kukabiliane nayo ni kupambana na makundi ya kigaidi yanoyojihusisha na matumizi ya nguvu."
Mwaka jana uwanja wa ndege wa Ataturk mjini Istanbul ni uwanja ulioshika nafasi ya 11 kwa kuwa na harakati nyingi sana duniani kwa kuwahudumia abiria milioni 61.8
Mwandishi : Mohamed Dahman/AP/dpa
Mhariri :Yusuf Saumu