1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki kuwaondosha raia 200 walionaswa chini ya ardhi Gaza

10 Novemba 2025

Uturuki inasema inapigania kuwaondosha raia wapatao 200 walionasa kwenye mahandaki katika Ukanda wa Gaza, baada ya kufanikisha kurejeshwa kwa mwili wa mwanajeshi wa Israel aliyeuawa zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Israel Tel Aviv 2025 | kaka wa Hadar Goldin
Chemi Goldin, kaka wa mwanajeshi Hadar Goldin, akizungumza kwenye mkutano kabla ya mabaki ya mwili wa ndugu yake kurejeshwa kutoka Gaza.Picha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Afisa wa ngazi za juu wa Uturuki alisema nchi yake imefanikisha kurejeshwa kwa mabaki ya mwili wa Hadar Goldin baada ya juhudi za kina "zinazoakisi dhamira njema ya kundi la Hamas" kwenye mpango wa kusitisha mapigano.

Hata hivyo, afisa huyo aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kinachofuatia sasa ni kuwahakikishia raia hao walionasa kwenye njia za chini ya ardhi huko Gaza  wanatoka salama.

Hayo yakijiri, kundi la Hamas lilisema wapiganaji wake waliozungukwa kwenye eneo la Rafah linaloshikiliwa na Israel wasingesalimu amri, na badala yake limewataka wapatanishi kusaka suluhisho la mzozo huo unaoweza kuhatarisha usitishaji mapigano. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW