Uturuki yashambulia kaskazini mwa Iraq
25 Desemba 2007SULAIMANIYA
Ndege za kivita za Uturuki zimeshambulia ndani ya eneo la Iraq karibu na mpaka wake hii leo lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa kufuatia shambulio hilo.
Kanali Hussein Tamar mkuu wa jeshi linalosimamia eneo la mpaka katika mkoa wa wakurdi wa Dahuk chini Iraq amesema shambulio hilo lililenga sehemu ambayo watu walihama mapema mwezi huu.Uturuki imekuwa ikishambulia kaskazini mwa Iraq katika miezi ya hivi karibuni kwa lengo la kuwaangamiza waasi wa chama cha PKK.Inadaiwa Uturuki imekuwa ikisadiwa na wanajeshi wa Marekani ambao wamekiri wamekuwa wakitoa nafasi kwa ndege za Uturuki kutumia anga hizo.Aidha wanajeshi wa ardhini wa Uturuki wamekuwa baadhi ya wakati wakivuka mpaka na kuvamia kaskazini mwa Iraq.Uturuki inadai inahaki ya kuwasaka waasi wa chama cha PKK kaskazini mwa Iraq.