1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yataka Israel ishinikzwe juu ya mpango wa amani Gaza

24 Oktoba 2025

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema Marekani na mataifa mengine yanapaswa kuchukua hatua zaidi kuishinikiza Israel kusitisha ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza.

Uturuki Ankara | Rais wa Uturuki
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan Picha: DHA

Akiwa njiani kurejea kutoka Oman, Erdogan alisema kundi la Hamas linaheshimu makubaliano hayo, na kwamba Uturuki iko tayari kuunga mkono kikosi kazi kinachopangwa kwa ajili ya Gaza.

Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alisema hatua nzuri zimepigwa katika utekelezaji wa mpango wa amani wa Marekani kwa Gaza, na kueleza matumaini kwamba mazungumzo hayo yataendelea kuleta matokeo chanya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW