1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yatetea mashambulizi dhidi ya PKK.

19 Desemba 2007

Ankara.

Uturuki imetetea mashambulizi yake ya kijeshi ndani ya eneo la kaskazini mwa Iraq dhidi ya waasi wanaotaka kujitenga wa Kikurd. Mashambulizi hayo ndani ya mpaka wa nchi hizo mbili yalitokea jana wakati wanajeshi wapatao 300 wa Uturuki waliposhambulia maeneo ya waasi ndani ya ardhi ya Iraq.

Hatua hiyo imekuja licha ya onyo kutoka kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice kuwa hatua ya kijeshi ya Uturuki inaweza kuathiri zaidi eneo hilo. Iraq pia imesema kuwa hatua za kijeshi za hapo baadaye zinapaswa kuratibiwa na utawala wa Baghdad.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW