1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yakiri kukutana na Urusi na Iran kuijadili Syria

6 Desemba 2024

Uturuki imethibitisha leo kuwa itakutana nchini Qatar na mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Iran kwa ajili ya kufanya mazungumzo juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Hakan Fidan
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki Hakan Fidan Picha: DHA

Chanzo kutoka wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imesema Waziri Hakan Fidan atakutana na mawaziri wenzake wa Urusi na Iran kwa mkutano chini ya mchakato wa Astana, kandokando na kongamano linalofanyika mjini Doha, kesho Jumamosi.

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa mkutano huo utafanyika kati ya Uturuki, inayounga mkono baadhi ya makundi ya waasi nchini Syria na washirika wa Damascus, Iran na Urusi.

Umoja wa Mataifa watoa wito wa kupunguza uhasama Syria

Mchakato unaojulikana kama Astana, unaozihusisha nchi hizo tatu, ulianzishwa na Kazakhstan mwaka 2017 kwa lengo la kupata suluhisho la kisiasa kwa vita nchini Syria, vilivyoibuka upya baada ya kundi la waasi wenye itikadi kali za dini kufanya mashambulizi ya ghafla ikivilenga vikosi vya usalama vya serikali.

Qatar ambayo mwanzoni iliunga mkono waasi baada ya serikali ya Rais Bashar al-Assad kuzima maandamano ya amani mwaka 2011, imesalia kuwa mkosoaji mkubwa wa Assad japo inatoa wito wa kumalizwa kwa vita hivyo  kwa njia ya mazungumzo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW