1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yatoa mwito kwa PKK kuweka chini silaha

1 Machi 2008

ANKARA:

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa mwito kwa waasi wa Kikurdi wa chama cha PKK kilichopigwa marufuku,kuweka chini silaha.Amesema,hakuna kinachoweza kupatikana kwa kutumia ugaidi.Wito huo ulitolewa muda mfupi baada ya serikali ya Uturuki kutangaza hapo siku ya Ijumaa kuwa imekamilisha operesheni yake dhidi ya waasi hao kaskazini mwa Irak.Kwa mujibu wa mkuu wa majeshi ya Uturuki,zaidi ya wanamgambo 240 wa PKK na wanajeshi 27 wa Uturuki waliuawa katika mapambano hayo.