Uturuki yatuma wataalam kusaidia kutafuta miili Gaza
17 Oktoba 2025
Uturuki imetuma timu ya wataalam wa kushughulikia majanga kusaidia kutafuta miili iliyo chini ya vifusi huko Gaza, wakati Rais Donald Trump wa Marekani akitoa onyo kwa Hamas juu ya mfululizo wa mauaji ya hivi karibuni katika eneo hilo.
Trump ameyataja mauaji hayo kama ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano aliyoyaongoza, ambapo kundi la wanamgambo la Hamas liliwarudisha mateka 20 wa mwisho walionusurika kwa Israel. Hamas imedai kuwa imerejesha miili yote ya mateka lakini miili 19 bado haijulikana iliko na inaaminika kufunikwa chini ya magofu pamoja na idadi kubwa ya Wapalestina.
Hamas imesema kuwa inaheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel na wanataka kurejesha miili yote ya mateka iliyosalia Gaza. Wataalam wa Uturuki watasaidia kuitafuta miili ya mateka huku familia zikikasirishwa na Hamas kwa kushindwa kurejesha miili ya jamaa zao.