1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yawakamata watu 15 waliowashambulia Wamarekani

Josephat Charo
3 Septemba 2024

Uturuki imewatia mbaroni watu 15 wanaotuhumiwa kwa kuwashambulia wanajeshi wa Marekani katika mji wa Izmir

Manuwari ya kivita ya Marekani, USS Wasp
Manuwari ya kivita ya Marekani, USS WaspPicha: ANKA

Uturukiimewakamata wanachama 15 wa vuguvugu la kizalendo la vijana linalotuhumiwa kwa kuwashambulia na kuwapiga maafisa wa jeshi la wanamaji la Marekani katika mji wa magharibi wa Izmir. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na maafisa.

Waliokamatwa ni wanachama wa kundi linaloipinga sana Marekani la Turkish Youth Union, TGB, ambalo wanachama wake wamewahi kufanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa jeshi la wanamaji la Marekani.

Mabaharia hao ni sehemu ya wafanyakazi wa meli ya kivita ya Marekani USS Wasp ambayo imetia nanga Izmir tangu Septemba mosi.

Vuguvugu la TGB limedai kuhusika na shambulizi hilo likisema wanajeshi wa Marekani wenye damu ya wanajeshi wao na damu ya maalfu ya Wapalestina mikononi mwao hawawezi kuinajisi nchi yao. Tukio hilo limewaghadhabisha wengi nchini Uturuki.