1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Uturuki yazindua manuari kubwa ya kijeshi

Hawa Bihoga
11 Aprili 2023

Uturuki imezindua manuari ya kijeshi ilioundwa kubeba zana kadhaa za kijeshi ikiwa ni pamoja na ndege zisizokuwa na rubani,magari zadi ya 90, pamoja na vifaru visivyopungua 10.

Türkei I Panzer
Picha: Fatih Aktas/AA/picture alliance

Rais Recep Tayyip Erdogan,ambae yupo kwenye kampeni za kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Mei amesema, manuari hiyo itaisaidia Uturuki kufanya operesheni za kijeshi na za kiutu katika pande zote za ujia wa bahari, ikiwa italazimika kufanya hivyo.

Uturuki ambe nimwananchama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ameonekana kuimarisha zaidi sekta yake ya ulinzi kwa miaka ya hivi karibuni huku Ankara ikijivunia mafanikio ya ndege zake zisizo na rubani.

Ndege hizo zilizotengenezwa na Uturuki na kampuni ya Baykar zilitumiwa na Kyiv katika saa za mwanzoni za uvamizi wa Urusi mwaka jana, huku mara kadhaa ikifanya juhudi za upatanishi kati ya Kyiv na Moscow.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW