1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwekezaji Tanzania waathiriwa na corona

Admin.WagnerD29 Aprili 2021

Kituo cha uwekezaji nchini Tanzania kimesema idadi ya miradi ya uwekezaji imepungua nchini humo kutokana na athari za janga la virusi vya corona zinazoshuhudiwa kote ulimwenguni.

Tansania | Amtseinführung Präsidentin Samia Suluhu Hassan
Picha: AP Photo/picture alliance

Kituo cha uwekezaji nchini Tanzania kimesema, idadi ya miradi ya uwekezaji imepingua nchini humo kutokana na athari za janga la virusi vya corona duniani, hatua ambayo imechangia kuzorotesha upatikanaji wa ajira mpya ambazo zilikuwa zinategemewa kupatikana katika kipindi kama hiki. 

Katika kipindi kama hiki mwaka uliopita taasisi hiyo ilio chini ya serikali na inayojiendesha kwa kutegemea sera za uchumi za nchi, ilifanikiwa kusajili jumla ya miradi ya uwekezaji 169 iliyozalisha zaidi ya ajira 10,000, lakini katika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona hali imekuwa ni tofauti kwani ni miradi 150 pekee ndio iliosajiliwa huku kiwango cha ajira zilizozalishwa kikiwa hakijafikia lengo.

Kati ya miradi iliyosajiliwa viwanda ndio vinashika hatamu ambapo miradi 30 imesajiliwa sawa asilimia 59, huku sekta ya utalii ikizalisha ajira kwa kiwango cha asilimia 13 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu.

Kituo cha mabasi ya Mbezi Luis umekuwa moja ya miradi mikubwa ya uwekezaji katika jiji la Dar es Salaam.Picha: Eric Boniphace/DW

Mkurugenzi mkuu wa kituo cha uwekezaji nchini dokta Maduhu Kazi amewaambia waandishi wa habari kwamba nchi mbalimbali zinashuhudia makali ya janga la corona lenye matokeo ya kuendelea kuvuruga uchumi wa dunia, mitaji ya wawekezaji nayo imekuwa ikishuka.

Soma Zaidi: Mzozo wa madereva wa malori Dangote kutafutiwa suluhu

Kwa mujibu wa taarifa ya dunia ya uwekezaji kwa mwaka 2020 mwenendo wa uwekezaji kutoka nje umepungua kwa kiwango cha asilimia 2, huku sababu ikiwa ni kupungua kwa mwenendo wa ukuaji wa uchumi na uhitajio wa bidhaa ghafi.

Aidha, amewagusia watanzania wanaoishi ughaibuni, akisema umefika wakati kwa kundi hilo kuangaliwa kwa kuwa limekuwa na mchango mkubwa kiuchumi pale wanapotuma fedha nyumbani kwa ajili ya shughuli za maendeleo, na kutaka dhana kuwa watu hao si wazalendo iachwe.

Baadhi ya watu wanaoishi nje ya Tanzania (wanadiaspora) wameiambia DW kuwa uwekezaji wao ni mkubwa na wa uhakika, isipokuwa kukosekana kwa sera inayowatambua wao na mchango walionao kunasababisha wengi kuhisi wanabaguliwa na kukata tamaa. 

Sikiliza Zaidi: 

TIC yasema mazingira ya uwekezaji Tanzania sasa safi

This browser does not support the audio element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW