1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwekezaji wa China nchi Angola wachukiza raia

10 Julai 2015

Wakati suala la kupunguza bei ya mafuta kwa nusu lilisababisha pengo katika akiba ya fedha ya Angola, ilijulikana wazi nchi hiyo inayoshika nafasi ya tatu kwa uchumi mkubwa kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

José Eduardo dos Santos Angola Präsident
Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos.Picha: Reuters

Nchi wa Angola mwaka huu, ilikuwa inahitaji msaada wa haraka na Rais Jose Eduardo dos Santos alijua wapi pa-kugeukia . Kiongozi huyo alielekea China. Lakini mikopo ya mabilioni ya dola iliyosaniwa na China mwezi uliopita imewakasirisha raia wa Angola.

Raia hao wa Angola wanasema wameachwa nyuma wakati wanasiasa na China wakigawana faida,huku taifa hilo la pili kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika likiendelea kuitegemea zaidi China.China imeipa Angola dola zipatazo bilioni 20 kwa miaka 27 ya vita vya wenyewe vilivyomalizika mwaka 2002, kulingana na makadirio ya shirika la habari la Reuters.

Malipo hayo mara nyingi hulipwa kwa mafuta au fedha kwenda moja kwa moja kwenye Makampuni ya ujenzi ya China ambayo yamejenga barabara, hospitali, nyumba na reli katika nchi zote za kusini mwa Afrika.Hii ina maana, hata hivyo, dola haziendi moja kwa moja kwenye uchumi wa nchi hiyo na hivyo kuongeza gharama za matumizi kwa wananchi wa kawaida wa Angola.

Uwepo wa polisi umeongezeka katika barabara za Luanda kutokana na mashaka ya umma na upinzani kuhusu ni kiasi gani serikali inaweza kuyakubali maslahi ya China katika juhudi yake ya kuimarisha uchumi ulioathiriwa na bei za chini za mafuta yasiyosafishwa.

Picha: AP

Watu kadhaa walikamatwa mnamo Juni 20 kwa madai ya kupanga maandamano ya kutishia "amani na usalama wa umma" kufuatia ziara ya rais dos Santos nchini China. Kundi la wapiganaji la FLEC ambalo linataka uhuru wa jimbo la kaskazini la Cabinda, lenye utajiri wa mafuta, lilitaka China iwaondoe raia wake wote kutoka eno hilo katika kipindi cha miezi miwili la sivyo "wataadhibiwa vikali".

Wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema Angola ina jeshi imara katika eneo la kusini mwa jangwa la sahara na hivyo upinzani wa aina yoyote kawaida hunyamazishwa haraka na kwa njia ya kikatili, hivyo basi kufanya iwe vigumu kuonyesha upinzani wa aina yeyote kwa serikali.

Ushawishi wa China barani Afrika kila mara hukosolewa na serikali za magharibi na baadhi ya viongozi wa Afrika wanaoiita ukoloni mambo leo, kwa kuchukua raslimali na badala yake kujenga miundo mbinu ambayo inachangia katika kuvifaidisha viwanda vya ujenzi vya China:

Kuna karibu makampuni 50 ya serikali ya Kichina na makampuni 400 binafsi yanayofanya kazi nchini Angola.Ambayo yanatakiwa kutumia asilimia 30 ya ajira za Angola lakini chanzo kimoja kilisema kuwa aliona mara chache raia wa Angola wakipata kazi katika nafasi za chini.

" Daima wachina wanakuwa waongozaji na waangola wanawakuwa wasaidizi , Hii ni nchi yetu.Tunapaswa kuwa waongozaji"alisema Paulo Nascimento, mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni dereva teksi.

Makampuni ya Kichina yamekana kwa nguvu shutuma za unyonyaji, wakisema kuwa wameijenga zaidi Angola tangu vita vimalizike, kuliko wakosoaji wa Magharibi ambao wamekaakando.Meneja masoko wa kampouni ya simu ya China ZTE, pascal wang mwenye umri wa miaka 36 aliliambia Shirika la habari la Reuters, " hatuji hapa kufanya biashara tu, bali tunataka kuisaidia Angola."

Ukiondoa uwekezaji kutoka kwa koloni lake la zamani Ureno na uchimbaji mafuta maeneo ya mwambao mwa Angola unaofanywa na Marekani na mataifa makubwa ya Ulaya, serikali za Magharibi, wahisani na wawekezaji wameelekeza zaidi juhudi zao kwengineko barani Afrika. Kuna dalili hali hiyo huenda ikabadilika.

Mwandishi:SalmaMkalibala/RTRE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW