1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vance: Ulaya itachukua sehemu kubwa ya usalama wa Ukraine

21 Agosti 2025

Makamu wa rais wa marekani JD Vance amesema Ulaya italazimika kuchukua sehemu kubwa ya hakikisho la usalama kwa Ukraine.

Großbritannien RAF Fairford 2025 | US-Vizepräsident JD Vance bei Besuch auf britischem Luftwaffenstützpunkt
Picha: Henry Nicholls/AFP

Akizungumza na kituo cha habari cha Fox News, Vance amesema Marekani inastahili kusaidia tu inapohitajika iwapo hilo litasaidia kumaliza mapigano.

Haya yanafanyika wakati ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Johann Wadephul amesema ni Urusi na Ukraine wanaostahili kuamua watakapokutana Rais Vladimir Putin na Volodymyr Zelenskiy kwa mkutano wao wa ana kwa ana.

Wadephul ameyasema haya huku uvumi ukizidi kwamba huenda viongozi hao wakakutana mjini Budapest.

Wadephul vile vile amekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na uwezekano wa kuhusika kwa majeshi ya Ujerumani katika kutoa hakikisho la usalama kwa Ukraine kama sehemu makubaliano yoyote ya amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW