VAR ni gumzo Uingereza yatengeneza au yaharibu?
11 Novemba 2019Katika ligi ya England, matumizi ya mfumo wa kumsaidia mwamuzi VAR katika Premier League umezua tafarani baada ya nia ya kumsaidia mwamuzi kutoa maamuzi sahihi na haki kwa timu, umeingia sasa katika mjadala mkuu iwapo ni sasa kuutumia ama la. Badala ya kuleta unafuu unaleta hali ya mkorogano wa maamuzi.
Badala ya kuondoa utata, maafisa wa VAR na marefa wanaonekana kuzidisha tatizo badala ya kutatua kutokana na maamuzi yao.
Mwishoni mwa juma kulikuwa na maamuzi kadhaa ya utata ,yakihusisha bao la Sheffield United dhidi ya Tottenham Hotspur siku ya Jumamosi na pia jana katika mchezo wa mafahali wawili Liverpool na Manchester City.
Kuna mambo kadhaa ya kiufundi ambayo yanaweza kujadiliwa baada ya ushindi wa Liverpool wa mabao 3-1 dhidi ya Manchester City.
Kocha wa Liverpool Juergen Klopp alisema baada ya mchezo huo:
"Naupenda mchezo, napenda hali mchezoni, ilikuwa safi sana. Watu, walikuwa katika hali ya kushangaza. na hasa dhidi ya wapinzani imara. nilisiki kila mtu akiniuliza kuhusu hilo. Sijaona bado. Penalti ana kushika kwa mkono kabla ya Ferbinho kufunga, kwa hiyo siwezi sema chochote juu yake. Lakini nilisikia ulikuwa mkono wa Bernardo Silva, sijui, lakini naweza kufikiria kuwa sio hali ambayo Pep anaifurahia. Hiyo ni kawaida.
Kuna mengi ya kujadili katika mchezo huo lakini kulikuwa na kitu kimoja dhahiri katika kikosi cha Juergen Klopp dhidi ya mabingwa watetezi ni kimwili walikuwa na nguvu. katika michezo ambayo City inadhibiti mpira na kuwakimbiza wapinzani kwa pasi zao za kijanja, ilionekana kimsingi ni kwa kiasi gani timu yao ilikuwa ndogo lakini wakati Liverpool inadhibiti kikosi cha Pep Guardiola kwa uwezo wa nguvu, ukosefu wao wa misuli ulionekana dhahiri. Katika mchezo wa jana Pep Guardiola amejifunza jambo.
"Nadhani leo tumeonesha katika uwanja mgumu kabisa duniani sababu kwanini sisi ni mabingwa. Kwa hiyo , moja kati ya mchezo mzuri kabisa tuliowahi kuonesha nikiwa kama meneja katika wakati huu katika uwanja huu. Sina la kusema. Bahati mbaya tumepoteza. Hongera Juergen na timu yake bora ya Liverpool kushinda , 3-1. Nafikiri ulikuwa mchezo mzuri kwa timu zote, kwa ajili ya Premier League, kwa mabilioni ya watu ambao waliuangalia mchezo huo."
Kocha wa Liverpool Juergen Klopp amesema ni mapema mno kuzungumzia juu ya ubingwa wa ligi na mwenzake wa Manchester City Pep Guardiola anaendelea kujipa moyo licha ya kipigo.
Mshindi mara tatu wa taji la Premier mlinzi Jonny Evans amechukua hatua ya kutuliza mzuka wa mashabiki wa Leicester City kwamba klabu hiyo inaweza kurudia kile ilichokifanya wakati waliponyakua taji hilo mwaka 2016 akisema kipindi cha heka heka cha wakati wa Krismas kitatoa picha halisi zaidi. Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 31 kutoka Ireland ya kaskazini ambaye ameshinda mataji matatu ya ligi akiwa na Manchester United, amekuwa na jukumu muhimu katika kikosi cha Mbweha hao msimu huu chini ya kocha kutoka Ireland pia Brendan Rodgers.