Vatican yatuma mjumbe Moscow
27 Juni 2023Matangazo
Hayo yameelezwa leo kupitia taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Kanisa Katoliki mjini Vatican.
Safari hiyo ya siku mbili ya Kadinali Matteo Zuppi mjini Moscow inafanyika wakati ikulu ya Kremlin inasawazisha hali ya mashaka iliyotokana na jaribio la uasi lililofanywa na kundi la mamluki la Wagner siku chache zilizopita.
Soma zaidi: Papa Francis akanusha kuwa anapanga kujiuzulu hivi karibuni
Taarifa ya Vatican imesema Kadinali Zuppi ambaye tayari aliitembelea Ukraine mwezi uliopita, ataambatana na afisa mmoja wa sekretariati ya Vatican kwenye safari hiyo nchini Urusi.
Lengo la ziara yake ni kuhimiza pande zote kujali ubinadamu na hataimaye kupata njia za kumaliza mzozo na kurejea kwa amani.