1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VATIKAN: Papa asikitika kuwaudhi Waislamu

16 Septemba 2006

Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amesema anasikitika kuwa hotuba yake iliyogusia Uislamu,imewaudhi waislamu.Katika hati iliyosomwa na afisa wa ngazi ya juu katika Vatikan,Papa amesema,anaheshimu Uislamu na ni matumaini yake kuwa Waislamu wataelewa maana halisi ya maneno yake.Siku ya Jumanne,wakati wa ziara yake nchini Ujerumani,Papa alimnukuu mfalme wa Byzantine wa karne ya 14 aliesema kuwa Mtume Muhammad hakuleta cho chote kile duniani isipokuwa uovu.Matamshi hayo yamewahamakisha Waislamu sehemu mbali mbali za dunia.Magazeti ya Kiarabu yametoa mwito kwa mkuu wa Kanisa la Kikatoliki binafsi kuomba msamaha kwa matamshi hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW