SiasaVenezuela
Venezuela: Marekani imeanza kuziachia fedha ilizozizuia
28 Januari 2026
Matangazo
Rodriguez ambaye alichukua hatamu za uongozi wa nchi hiyo baada ya makomandoo wa Marekani kumkamata na kumwondoa madarakani Maduro mnamo Januari 03, ametoa taarifa hiyo kupitia hotuba kwa taifa jana Jumanne.
Serikali ya Venezuela imekuwa chini ya vikwazo vya kiuchumi vya Marekani ikiwemo marufuku ya kuuza mafuta tangu mwaka 2019 baada ya Washington kuutilia mashaka ushindi wa Maduro kwenye uchaguzi wa mwaka 2018.
Wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Donald Trump, Marekani ilizuia pia fedha za Venezuela zilizowekwa kwenye akaunti za kimataifa ambazo serikali mjini Caracas ilikadiria kuwa thamani yake inafikia dola bilioni 30.