1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela na Ecuador zapinga uvamizi wa Colombia dhidi ya FARC

3 Machi 2008

Nchi hizo zimepeleka wanajeshi katika mipaka yake kuzuia harakati za wanajeshi wa Colombia

CARACAS

Rais Hugo Chavez wa Venezuela amepeleka vifaru vya kijeshi na maelfu ya wanajeshi katika eneo la mpaka baina ya nchi yake na Colombia kufuatia uvamizi uliofanywa na jeshi la Colombia katika kambi ya waasi wa kundi la FARC iliyoko kwenye msitu wa eneo hilo ndani ya nchi ya Ecuador. Rais Chavez ameionya serikali ya Colombia ambayo ni mshirika wa Marekani kwamba Venezuela haiwezi kuruhusu kitendo kingine kama kile cha kuuwawa kiongozi wa juu wa kundi hilo la waasi wa Farc Raul Reyes na wapiganaji wengine 16 ambao waliuwawa katika uvamizi wa jumamosi.

Ecoudor pia imejibu juu ya uvamizi huo wa Colombia kwa kumtimua balozi wa nchi hiyo na kumuondoa balozi wake nchini Colombia pamoja na kupeleka wanajeshi katika mpaka wake ili kupinga dhidi ya kile ilichokitaja kuwa ni uvamizi usiokubalika.Hata hivyo Colombia kwa upande wake imesisitiza kwamba haijakiuka sehria zozote dhidi ya utawala wa Ecoudor kwa sababu shughuli za wanajeshi wake zilifanyika kihalali kwa lengo la kuilinda nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW