Venezuela wapiga kura kumchaguwa mpinzani wa Maduro
22 Oktoba 2023Uchaguzi huo wa siku ya Jumapili (Oktoba 22) ulifanyika wakati Marekani ikitowa ahadi ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo iwapo serikali itashindwa kuondoa marufuku inayowabana baadhi ya wanasiasa wa upinzani kushikilia nafasi za serikali.
Maria Corina Machado, aliye na miaka 56, mhandisi na mbunge wa zamani alitajwa kuongoza kwa alama 40 mbele ya wapinzani wake.
Soma zaidi: Marekani kulegeza vikwazo vya mafuta na gesi dhidi ya Venezuela
Lakini Machado kama ilivyokuwa kwa waliokuwa wapinzani wawili wa Maduro, haruhusiwi kushikilia nafasi katika ofisi za umma kufuatia kuunga mkono vikwazo ilivyowekewa serikali ya Maduro na Marekani na hataweza kujisajili kushiriki uchaguzi mkuu.
Soma zaidi: Serikali, upinzani Venezuela wakubaliana uchaguzi mwakani
Machado aliyesema lengo lake ni kumshinda Maduro katika uchaguzi ulio huru, haki na wa amani, akisisitiza kuwa anaweza kuishinikiza tume ya uchaguzi kumuacha ajisajili.
Rais Maduro hajatangaza nia yake ya kugombea, lakini waangalizi wengi wanamtarajia kufanya hivyo.