1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Venezuela yawakataa waangalizi wa EU katika uchaguzi wake

29 Mei 2024

Venezuela imekataa kuwaalika waangalizi wa uchaguzi wa rais kutoka Umoja wa Ulaya, ikiishinikiza Jumuiya hiyo iondowe vikwazo vyake ilivyoiwekea.

Nicolas Maduro - Venezuela
Rais wa Venezuela Nicholas Maduro Picha: Marcelo Garcia/AFP

Mkuu wa tume ya uchaguzi Elvis Amoroso jana aliutaka Umoja wa Ulaya uondowe vikwazo vyote na kufuta kile alichosema ni msimamo wa chuki dhidi ya Venezuela.

Amesema tume hiyo imechukuwa uamuzi huo kwa misingi ya kulinda uhuru na mamlaka ya taifa hilo kufuatia uharibifu uliotokana na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa mwaka 2017. 

Uchaguzi Mkuu unaosubiriwa Venezuela kufanyika mwezi Juni

Nchi za Umoja wa Ulaya ziliiwekea nchi hiyo vikwazo kadhaa ikiwemo kuwapiga marufuku kusafiri kwenye jumuiya hiyo maafisa  54 na kuzuia mali zao,kwa kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu na kuhujumu demokrasia na utawala wa sheria nchini Venezuela.

Uchaguzi wa rais utafanyika Julai 28 na rais Nicolas  Maduro atagombea muhula wa tatu akipambana na mwanadiplomasia wa muda mrefu Edmundo González Urrutia kutoka muungano wa upinzani wa Unidad Venezuela. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW