Venezuela yatoa picha za rais Chaves
16 Februari 2013Taarifa mbalimbali zilisema rais huyo wa kisoshalisti, Hugo Chaves ana shida ya kupumua na kwamba anapumua kutumua vifaa maalumu na akiwa na shida ya kupumua. Picha hizi zilizotolewa sasa zinaonamuonesha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58 akitabasamu lakini sura yake ikiwa kama imevimba. Alikuwa amelala kaitika kitanda cha hosiptali huku mabinti wake wawili wakiwa pembeni na mwenyewe akisoma gazeti la serikali la Cuba Granma.
Maelezo kuhusu Chaves
Picha hizo zilitolewa na mkwe wa Chaves, Waziri wa Sayansi Jorge Arreaza, ambae amekuwa akisafiri mara kwa mara kati ya Havana na Caracas kwa lengo la kuwa karibu na kiongozi huyo wa Venezuela. Akizungumza kupitia televisheni ya taifa waziri huyo amesema Chavez kwa sasa hana ile sauti yake ya kawaida. Anakuwa na wakati mgumu katika kuzungumza lakini anaweza kuelewa mambo. Anaweza kuwasilisha umuzi wake vyema. Na kuweza kuandika vyema.
Chavez hakuonekana hadharani, na mpaka sasa halijasikiwa lolote kutoka kwake tangu alipofanyiwa upasuaji wa nne uliyotokana na ugonjwa wa saratani Desemba 11, mwaka jana. Hata hivyo mpaka sasa sio picha hizo wala kutolewa taarifa madhubuti inayoweza kuonesha kama kiongozi huyo anaweza kurudi nyumbani au kulazimika kujiuzulu.
Makamu wa rais wa Venezuela ambae ndie anaekaimu nafasi ya urais Nicolas Maduro, alinukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema rais Chaves yupo katika wakati mgumu sana ingawa hakutoa maelezo yoyote.
Mwandishi: Sudi Mnette/RTR
Mhariri:Sekione Kitojo