1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Verdi yaitisha mgomo Ujerumani wa kushinikiza masharti yao

15 Februari 2023

Wahudumu katika viwanja saba vya ndege nchini Ujerumani, vikiwemo vyenye shughuli nyingi vya Frankfurt na Munich, watafanya mgomo wa siku moja Ijumaa ili kushinikiza masharti yao ya nyongeza ya mishahara.

Frankfurt am Main | Verdi-Warnstreik bei Lufthansa
Picha: Timm Reichert/REUTERS


Mgomo huo unatarajiwa kusababisha kucheleweshwa na kufutwa safari kwa maelfu ya abiria, hasa wale wa safari za ndani. Chama cha wafanyakazi Ujerumani - Verdi kimesema wafanyakazi wanaongeza mbinyo kwa waajiri wao kwa sababu mazungumzo mpaka sasa hayajaleta suluhisho.

Lufthansa yafuta karibu safari zote za ndege sababu ya mgomo

Chama cha Verdi kwa sasa kinaongoza mazungumzo kwa niaba ya wafanyakazi wa sekta ya umma, wahudumu wa viwanja vya ndege na wafanyakazi wa usalama wa safari za angani, wakidai mishahara mizuri katika wakati ambao wanashuhudia mapato yao yakipungua kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Wafanyakazi wa Lufthansa waendelea na mgomo

Mgomo huo wa siku moja utaathiri viwanja vya ndege katika miji ya Bremen, Dortmund, Frankfurt, Hamburg, Hanover, Munich na Stuttgart.