1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Verstappen ashinda Azerbaijan Grand Prix

13 Juni 2022

Na katika mbio za magari ya Formula One, Max Verstappen kwa mara nyingine tena aliyatumia vyema matatizo ya mpinzani wake Charles Leclerc katika kinyang'anyiro chao cha ubingwa wa dunia.

Aserbaidschan | Formel 1 | Grand Prix
Picha: Sergei Grits/AP Photo/picture alliance

Verstappen alitanua uongozi wake wa F1 kwa kushinda mbio za Azerbaijan Grand Prix jana, ukiwa ni ushindi wake wa tano wa msimu baada ya tukio jingine la Leclerc kujiondoa mapema kutokana na matatizo ya injini.

Sergio Perez dereva mwenza wa Verstappen katika kampuni ya Red Bull alimaliza wa pili huku George Rusell wa Mercedes akipanda jukwaani katika nafasi ya tatu. Bingwa mara saba wa ulimwengu Lewis Hamilton alimaliza wa nne.

afp

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW