1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vettel na Leclerc wagongana na kutolewa katika Grand Prix

Sekione Kitojo
18 Novemba 2019

Madereva wa magari ya Ferrari Sebastian Vettel na Charles Leclerc wamegongana wakiwania nafasi ya nne na waliondolewa katika mbio za Brazil Grand Prix.

Formel 1 - Großer Preis von Brasilien | Unfall Lewis Hamilton und Alexander Albon
Picha: Getty Images/AFP/D. Magno

 

Sebastian Vettel  na  Charles Leclerc wamekabiliana  na shutuma kali  kutoka  kwa  mkuu  wa  timu  ya  magari  hayo ya  Ferrari Mattia Bonotto  baada  ya   magari  yao  kugongana na  kuondolewa katika  mashindano  ya  jana  Jumapili  ya  Grand Prix  nchini  Brazil. Madereva  hao  walikuwa  wakiwania  kumalizika  katika  nafasi ya nne  wakati  walipogongana wakati Vettel  alilipiza  kisasi  kwa kupitwa  na dereva  mwenzake  wa  Ferrari.

Max Verstappen mshindi wa Brazil Grand PrixPicha: Getty Images/R. Cianflone

Max Verstappen ameweka  alama  yake  kama bingwa wa  hapo baadae  jana kwa  ushindi  kwa  magari  ya  Red Bull katika  mbio hizo  za  Grand Prix nchini  Brazil.

Kwa  taarifa  hiyo  ndio sina  budi  kusema  tumefikia  mwisho  wa habari  hizi  za  michezo  jioni  ya  leo, tutembelee  katika  ukurasa wetu wa  michezo, kwa  habari  zaidi  katika dw.com, michezo, jina langu  ni Sekione Kitojo, kwaheri.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW