1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mganda, Victor Kiplangat ashinda dhahabu, Marathon

27 Agosti 2023

Raia wa Uganda Victor Kiplangat ameshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Riadha ya Dunia kwa wanaume yaliyofanyika Jumapili hii huko Budapest.

Ungarn Budapest | Budapest World Athletics - Victor Kiplangat gewinnt Marathon
Picha: Kunihiko Miura/AP/picture alliance

Victor Kiplangat mwenye miaka 23 alikimbia kwa muda wa saa mbili, dakika 8 na sekunde 53.

Mwanariadha huyo aliyeshinda pia medali ya dhahabu mwaka 2022, katika michuano ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, alifanikiwa kumaliza akiwa bado na sekunde 19.

Mshindi wa pili Maru Teferi raia wa Israel alijishindia medali ya fedha na Leul's Gebresilase kutoka Ethiopia akishinda nafasi ya tatu na kushinda medali ya shaba.

Kiplangat alisema baada ya kumaliza mbio hizo kwamba haikuwa rahisi na hasa kutokana na hali ya joto kali, ingawa amesema lijiandaa kisaikolojia kukabiliana na changamoto hiyo, na kuongeza kuwa hiyo ilimfanya ajisikie kuwa na nguvu kila wakati.

Soma Pia:Kipchoge aweka historia katika mbio za marathon 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW