Victoria, Zimbabwe. Chissano mpatanisha wa mzozo wa kisiasa nchini Zimbabwe.
13 Agosti 2005Matangazo
Kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai ameukaribisha uteuzi wa rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chissano katika upatanishi wa mzozo mkubwa wa kisiasa katika Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru.
Umoja wa Afrika wiki hii ulimteua Chissano kufanya upatanishi kati ya chama cha rais Robert Mugabe cha Zanu PF na kile cha Morgan Tsvangirai cha Movement for Democratic Change MDC.