1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vieira ameshinda uchaguzi wa Rais Guinea Bissau

28 Julai 2005

Bissau:

Kwa mujibu wa matokeo rasmi, aliyekuwa mtawala wa kijeshi, Joao Bernardo Vieira, ameshinda uchaguzi wa Rais nchini Guinea Bissau. Lakini Wapinzani wake wamesema kuwa hawatatambua matokeo hayo. Muda mfupi baada ya Tume ya uchaguzi kutangaza matokeo hayo, wapinzani wakishika chupa na mawe wamepambana na Wafuasi wa Vieira katika barabara za mji mkuu, Bissau. Amani imerudi tena baada ya polisi kuingilia kati na kuwatawanya. Mnadhimu Mkuu wa majeshi amesema kuwa Wanajeshi wake hawatavumilia kitendo chochote kile kitakachovuruga amani. Taarifa ya jeshi imesema kuwa Wanajeshi watamchukulia hatua kali mtu ye yote yule au chama chochote kile atakayejaribu kuvuruga matokeo ya uchaguzi. Tume ya uchaguzi imetangaza kuwa kwa mujibu wa matokeo ya awali Vieira, anayejulikana kama „Nino“ amepata asili mia 55.25 ya kura. Mpinzani wake Malam Bacai Sanha wa chama kikubwa cha PAIGC amepata asili mia 44.75 ya kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW