1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA : Chombo kipya cha haki za binaadamu Ulaya

2 Machi 2007

Umoja wa Ulaya hapo jana umezinduwa wakala mpya wa haki za binaadamu wenye makao yake makuu mjini Vienna Austria kusaidia kufuatilia masuala ya ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni.

Kamishna wa Sheria wa Umoja wa Ulaya Franco Frattini amesema Umoja wa Ulaya wenye nchi wanachama 25 lazima uoanishe sheria zao kuzuwiya kinga ya hifadhi kwa wale wanaochochea chuki.Ametaja mfano wa shambulio la chuki dhidi ya Uyahudi mwishoni mwa juma katika shule ya chekechea ya Kiyahudi mjini Berlin kwa kusema kwamba Ulaya lazima itetee maadili yake ya msingi ya kuwepo kwa haki kwa wote.

Hapo Jumapili watuhumiwa wa Manazi mambo leo walichora kauli mbiu za kashfa kwenye kuta na kurusha bomu la moshi kwenye jengo la shule hiyo.Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amelaani tukio hilo kwa kusema kwamba shambulio hilo ni sawa na kushambulia demokrasia ya Ujerumani.

Makundi ya haki za binaadamu yanasema wakala huo mpya wa haki za binaadamu wa Umoja wa Ulaya utakuwa dhaifu mno kuweza kukabiliana na dhuluma za ukiukaji wa haki za binaadamu.